Upishi wa Visheti

Vipimo

 

Unga                                                   2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga         2 Vijiko vya supu

Maziwa                                               ¾ Kikombe

Iliki                                                      Kiasi

Mafuta ya kukarangia                        Kiasi

Shira

Sukari                                                 1 Kikombe 

Maji                                                   ¾ Kikombe

Vanila                                                 ½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda)                           Kiasi

maxresdefault IMG_4772 DSC07390

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.

1. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.

2. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.

3. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.

4. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.

5. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.

6. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *