Kabeji Ya Kukaanga

 VIPIMO:

Kabeji                                                          ¼ kabeji

Karoti                                                          2

Kitunguu                                                      2 viwili

Nyanya                                                        1

Nyanya ya kopo                                           1 kijiko cha chai

Pilipili mboga                                                 ½

Chumvi                                                        kiasi

Pilipili manga                                                 ½ kijiko cha chai

Bizari ya manjano                                        ¼ kijiko

Pilipili zilorowekwa katika siki

(hot pepper rings)                                        2 vijiko vya supu

Mafuta                                                         2 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata kabeji, karoti, vitunguu, pilipili mboga, nyanya weka kando.
  1. Tia mafuta katika karai kaanga vitunguu hadi vilainike na kuanza kugeuka rangi. Usiache vikageuka rangi sana.
  1. Tia nyanya, nyanya ya kopo, chumvi, pilipili manga, bizari, endelea kukaanga kidogo.
  1. Tia karoti endelea kukaanga kidogo.
  1. Tia kabeji na pilipili mboga kaanga kidogo tu.
  1. Zima moto na changanya na pilipili zilokatwakatwa na kurowekwa katika siki (hot pepper rings) ikiwa tayari kuliwa.

Mchicha Wa Bamia Na Sosi Ya Nyama

VIPIMO

Mchicha uliokatwa mdogomdogo                               600 gm

Bamia (kata ndogo ndogo)                                       2 Vikombe

Nyama ya ng’ombe kata vipande vidogodogo        2 LB

Thomu na tangawizi                                                 1 kijiko cha chai

Pilipili mbichi iliyosagwa (au nyekundu ya unga)    1 Kijiko cha chai

Vitunguu (kata vidogovidogo)                                  3

Nyanya (kata ndogo ndogo)                                    3

Nyanya ya kopo                                                       3 vijiko vya supu

Thomu iliyosagwa au kuparuzwa                           1 kijiko cha supu

Mafuta                                                                    ¼ kikombe

Chumvi                                                                    kiasi

Ndimu                                                                     1 kijiko cha supu

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 

1)     Chemsha nyama kwa maji ya kiasi, chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, na kitunguu kimoja. Hakikisha maji sio mengi ili itakapowiva ibakie supu yake kidogo tu.

2)     Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu mpaka viwe vyekundu kidogo, tia thomu kaanga kidogo tu.

3)     Tia nyanya kaanga mpaka zilainike, tia nyanya ya kopo.

4)     Weka mchicha na bamia endelea kukaanga.

5)     Mimina supu ya nyama, ongeza chumvi ikibidi, iwache kwenye moto kidogo kuwivisha mchicha na bamia.

6)    Tia ndimu.

7)    Mimina katika bakuli na ikiwa tayari kuliwa.

Mboga Mchanganyiko

VIPIMO:

Brokoli (Brocoli)                                                  1 mche

Karoti                                                                           3

Viazi                                                                              2

Njegere   (snow-peas)  au zozote                    1 kikombe

Zucchini (kama mamumnya)                              3

Pililipili mboga za rangi mbali mbali               1 kila rangi

Kidonge cha supu (Maggi cube)                            1

Pilipili manga                                                      1 kijiko cha chai

Chumvi                                                                kiasi

Sosi ya soy                                                         1 kijiko cha supu

Mafuta ya kukaangia                                           1/4 kikombe

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.       Kata kwanza viazi, zuchini na karoti vipande virefu verefu kisha chemsha  kidogo tu. Tia chumvi na pilipili manga.

2.      Tia mafuta katika karai, kaanga vitu vyote  isipokuwa brokoli na mapilipili makubwa.

3.       Karibu na kuwiva tia sosi ya soy na kidonge cha supu.

4.       Kata au chambua brokoli, kata kata mapilipili na tia katika mchangayiko, ipikike muda wa dakika tano tu. Changanya vizuri, tayari kuliwa na mkate au wali mweupe.

 

Kidokezo: 

 Usikaange au kuchemsha sana mboga  ili usipoteze vitamini zake.

Ndizi Mbivu

VIPIMO

Ndizi Mbivu                                       6

Nazi                                                  Kikopo 1

Sukari                                               Vijiko 3 vya chakula

Hiliki                                                 Kijiko 1

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1)     Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.

2)     Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.

3)     Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.

4)     Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi  na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.

5)    Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

 

KIDOKEZO:

Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.

Donate Button with Credit Cards

Pai Ya Viazi Na Nyama Ya Kusaga

Vipimo

Nyama ya kusaga                                      1½ lb (ratili)
Kitunguu                                                   1 Kikubwa
Thomu na tangawizi                                   1 Kijiko cha supu
Mboga upendayo
(karoti, mahindi, na kadhalika)                    1- 2 Kikombe
Viazi                                                          1½ – 2 lb (ratili)
Siagi                                                          ½ Kikombe
Kidonge cha supu kilichoyeyushwa               ½ Kikombe maji
Worcestershire sauce au yoyote nyingine      1 Kijiko
Chumvi                                                      kiasi
Mchanganyiko wa bizari                              1 Kijiko cha supu
Jibini (cheese) ya iliyochunwa (grated)        1 gilasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1.       Menya maganda ya viazi na katakata, kisha chemsha katika maji yenye chumvi hadi viwive.
2.       Wakati viazi vinaiiva, yeyusha nusu ya ile kipimo cha siagi katika sufuria kisha kaanga kitunguu hadi ilainike.
3.       Kisha tia thomu na tangawizi.
4.       Halafu tia nyama ya kusaga na ukaange hadi isiwe nyekundu tena.
5.       Weka mboga, chumvi na bizari zilizobakia na iachie moto mdogo kwa muda iive vizuri.
6.       Ponda viazi pamoja na ile siagi iliyobakia, kisha ongeza chumvi na pilipili manga ikiwa haijakolea.
7.       Tandaza kwanza viazi kisha mchanganyiko wa nyama katika treya ya oveni kisha tandaza tena viazi vilivyopondwa kwa kutumia uma ili iwe na dizaini upendayo.
8.  Mwagia jibini (cheese) juu yake.
9..       Pika katika oveni yenye moto wa 400° kwa muda wa dakika 30 hivi na ubadilisha moto wa juu katika dakika 5 za mwisho ili igeuke rangi ya kupendeza juu.
10..       Epua na tayari kuliwa.

Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu

Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,inafika mahala mpishi anahitaji pumzika na aondoke jikoni ata kwa siku kadhaa ili kuvuta pumzi.ndio maana majumbani mara moja moja familia hutoka na kwenda kula nje.

Leo sijaliona jiko tangu asubui,dada yangu aliamka mapema na kuandaa chai,na chakula cha mchana amekiandaa Rafiki yangu Hamida aliekuja kunisalimia baada ya kutoonana kwa muda mrefu.Kwa kua niliwai muomba anifundishe kupika Futari basi aliona leo ndio siku nzuri yakunifundisha.Baada ya kucheka kwingi,kula vitamu vya hapa na pale darasa la upishi wa futari lilianza.

 

Mahitaji

Mihogo

viazi vitamu

vitunguu maji

vitunguu swaumu

Tui la Nazi

Chumvi

Njia

1.Baada ya kumenya ,kuosha na kukatakata viazi na mihogo katika vipande vidogo vidogo.Weka viazi na mihogo ndani ya sufuria na uongeze maji yakutosha kuivisha,kisha funika na uchemshe

2.maji yakikaribia kuisha na mihogo na viazi vimeiva vizuri,ongeza chumvi,vitunguu maji na vitunguu swaumu kisha uchemshe adi vitunguu vilainike.

3.Ongeza Tui la nazi na uache vichemke adi nazi iive na mihogo na viazi viwe vimeiva kiasi cha kurojoka,usikaushe kwani chakula hichi chaitaji kua na utepea au urojo.

4.Epua jikoni na kiko tayari kwa kula,unaweza sindikiza chakula hiki na samaki au nyama yenye mchuzi na mboga ya majani pembeni ukipenda