Upishi wa Visheti

Vipimo

 

Unga                                                   2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga         2 Vijiko vya supu

Maziwa                                               ¾ Kikombe

Iliki                                                      Kiasi

Mafuta ya kukarangia                        Kiasi

Shira

Sukari                                                 1 Kikombe 

Maji                                                   ¾ Kikombe

Vanila                                                 ½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda)                           Kiasi

maxresdefault IMG_4772 DSC07390

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.

1. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.

2. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.

3. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.

4. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.

5. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.

6. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Upishi wa Tambi za Kukaanga

VIPIMO

Tambi                                        pakti moja

Sukari                                       ¾ kikombe cha chai

Mafuta                                       ½ kikombe cha chai

Iliki                                             kiasi 

Maji                                           3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose                    1-2 Tone

Zabibu                                       Kiasi (Ukipenda)

0112 0181 0391 Tambi za kukaanga

NAMNA YA KUTAYARISHA NA  KUPIKA

 

1.    Zichambue tambi ziwe moja moja.

2.    Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina  

      tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

3.    Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

4.    Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki  

      na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari

      koroga kidogo na punguza moto.

 5.    Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili  zikaukie vizuri. 

6.    Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

 

Kidokezi   Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza   kuongeza maji kidogo.

Upishi wa Kebabu

Wapishi wenzangu Asalaam Aleykum kwa cc waislam n Bwana acfiwe kwa upande wa pili.

Haya jongeeni kijiweni tuongezeane ujuzi wa mapishi. Angalia upishi wa KEBABU.

1

37

a4

65

Mahitaji

1. Nyama ya kusaga kl 1
2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu kimoja
3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
4. Swaum kikubwa kimoja n tangawizi
5. Mikate ile ya buku miwili ama mitatu
6. Chumvi kiasi
7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo sagwa
8. Pili pili hoho kubwa moja
9. Mafuta ya kupikia
10. Ndimu
11. Mayai sita

 

Kuandaa

Nyama ya kababu hua aichemshwi habisa. Kumbuka nyama kama ina maji kumbuka kuyakamua. Chukua nyama yako weka kwenye chombo kisafi, tia chumvi, ndimu, unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, alafu changanya huo mchanganyiko wako na uwakikiche umechanganyika vizuri kabisa.

 

Hatua inayo fuata.

Katakata vitunguu maji katika vipande vidogo vidogo kama vya sambusa vile, oya kotmili/giligilani zako vizuri na ukamue maji alafu toa ile mizizi ya nyuma na kisha katakata katika vipande vidogo vidogo, twanga swaum zako na badala ya hapo tia katika mchanganyiko wako ule wa nyama. Changanya mpaka uakikiche umechanganyika vizuri. Kuonja ruksa wapenzi iliuweze jua kama vitu vuote vipo sawa au laa….

Hatua ya tatu.

Chukua mikate yako toa ile nyama ya kati nikimaanisha ile nyama ya mkate nyeupe ule upindo wa pembeni ucweke sababu ni mgumu na co soft. Chambua mikate yako vizuri kabisa na inyambue nyambue na uweke katika mchanganyiko wako wa nyama, chukua mayai matatu uweke humo. Changanya vyote sasa kwa pamoja mpaka uwakikiche vimechanganyika ipasavyo. Na baada ya hapo utafanya kama unakanda unga wa ngano vilee na upate donge moja takatifu. Utaacha mchanganyiko wako kwa mda wa kama dk 10 or 15 hivi ili viungo viweze kukolea kwa uzuri.

Hatua ya nne na mwisho.

Kata vidonge vidodo vidogo ama upendavyo na kutengeneza style uipendayo, weka kwenye chombo safi, vyunja mayainyako yale matatu yalio baki na uweke kwenye bakuli toa vile viini vya ndani na ubaki na ute tu. Weka flampeni/karai lako jikoni na ucwe na moto mkali, moto uwe wa wastani tu, mafuta yako yakisha pata moto chukua kebabu zako tosa kwenye ule ute wa yai na uweke kwenye mafuta yakio jikoni na utarudia kwa vyote viduara ulivyo fanya. Baada ya hapo vitakua tayari kwa kuliwa. Ni tamuje sasa…..Very yummy waweza sukum7a na chochote Wallah.

Shurba Ya Nyama Ya Mbuzi

VIPIMO

 

 Nyama ya mbuzi ya mafupa au ya ng’ombe       Kilo moja

Mafuta                                                               2 vijiko vya supu

Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo)                   2

Nyanya (kata ndogo ndogo)                               1

Thomu na tangawizi iliyosagwa                           2 vijiko vya supu

Bizari ya pilau ya unga (Jeera)                            1 kijijo cha chai

Gilgilani ya unga (Dania)                                     ½  kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga                                          1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga                                              ¼ kijiko cha chai

Kotmiri (iliyokatwa ndogo ndogo)                       kiasi

Nanaa (iliyokatwa ndogo ndogo)                        kiasi

Chumvi                                                              kiasi

Siki                                                                    3 vijiko vya supu  

Shayiri (Oats) au *                                             2 vikombe

* ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa  muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive. 

   

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1.      Chemsha nyama na chumvi kwa maji kiasi  mpaka iwive

2.      Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.

3.      Weka bizari zote, pili pili manga, chumvi.

4.      Tia thomu na tangawizi.

5.      Tia nyanya na bila ya kuzikaanga sana tia nyama na supu yake.

6.      Tia kotmiri, nanaa.

7.      Pembeni changanya shayiri (oats) na maji koroga kisha tia katika supu ya shurba.

8.      Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.

9.      Tia siki na tayari kuliwa.

Supu Ya Kuku Na Viazi/Mbatata

VIPIMO :

Kuku                                                            4 LB

Viazi/mbatata                                              3

Kitunguu maji                                               1

Kitunguu thomu                                            5 chembe

Pilipili mbichi                                                  2

Nyanya ya kusaga                                       1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga                                    ½  kijiko cha chai

Haldi/tumeric/bizari ya manjano                    ¼  kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuni                                         2 vijiko vya supu

Kotmiri (coriander freshi)                              1 msongo

Ndimu/siki                                                    2 vijiko vya supu

Chumvi                                                        kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 1. Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
 1. Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.
 1. Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
 1. Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.
 1. Kisha  tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.
 1. Tia nyanya,  haldi, na maji kiasi.
 1. Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
 1. Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.
 1. Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa  na mkate au upendavyo

Viazi Vyekundu Vya Masala

VIPIMO :

Viazi /mbatata                                                       10 kiasi

Kitunguu maji kilichosagwa                                     1

Thomu iliyosagwa                                                  1 kijiko cha supu

Pilipili iliyosagwa                                                     1 kijiko cha chai 

Rai (mustard seeds)                                               1 kijiko cha supu

Majani ya mchuzi (curry leaves)                             7 majani

Uwatu uliosagwa (methi)                                       1 kijiko cha chai

Nyanya kopo                                                         5 vijiko vya supu

Ndimu                                                                    3 vijiko vya supu

Mafuta                                                                   ¼ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Chemsha viazi kiasi viwive lakini  visivurugike
 2. Menya, katakata vipande weka kando.
 3. Tia mafuta katika sufuria, yakishika moto tia rai, zikaange kwa muda wa dakika moja hadi zigeuke rangi kidogo.
 4. Tia majani ya mchuzi, uwatu, thomu, kitunguu maji, pilipili  kaanga kidogo tena.
 5. Tia nyanya kopo endelea kukaanga kidogo kisha tia chumvi, ndimu na maji kiasi kidogo ili kufanya rojo kiasi.
 6. Mimina viazi, changanya, pakua katika sahani.