Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu

Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,inafika mahala mpishi anahitaji pumzika na aondoke jikoni ata kwa siku kadhaa ili kuvuta pumzi.ndio maana majumbani mara moja moja familia hutoka na kwenda kula nje.

Leo sijaliona jiko tangu asubui,dada yangu aliamka mapema na kuandaa chai,na chakula cha mchana amekiandaa Rafiki yangu Hamida aliekuja kunisalimia baada ya kutoonana kwa muda mrefu.Kwa kua niliwai muomba anifundishe kupika Futari basi aliona leo ndio siku nzuri yakunifundisha.Baada ya kucheka kwingi,kula vitamu vya hapa na pale darasa la upishi wa futari lilianza.

 

Mahitaji

Mihogo

viazi vitamu

vitunguu maji

vitunguu swaumu

Tui la Nazi

Chumvi

Njia

1.Baada ya kumenya ,kuosha na kukatakata viazi na mihogo katika vipande vidogo vidogo.Weka viazi na mihogo ndani ya sufuria na uongeze maji yakutosha kuivisha,kisha funika na uchemshe

2.maji yakikaribia kuisha na mihogo na viazi vimeiva vizuri,ongeza chumvi,vitunguu maji na vitunguu swaumu kisha uchemshe adi vitunguu vilainike.

3.Ongeza Tui la nazi na uache vichemke adi nazi iive na mihogo na viazi viwe vimeiva kiasi cha kurojoka,usikaushe kwani chakula hichi chaitaji kua na utepea au urojo.

4.Epua jikoni na kiko tayari kwa kula,unaweza sindikiza chakula hiki na samaki au nyama yenye mchuzi na mboga ya majani pembeni ukipenda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *