Kinywaji:Strawberry shake

VIPIMO


Ndizi                                                     2 (wastani)

Stroberi (strawberries)                        Vikombe vya chai 2


Vipande vya barafu                             Kikombe cha chai 1


Maziwa                                               Kikombe cha chai  ¾ − 1 


Juisi ya machungwa                            Kikombe cha chai 1


Asali                                                    Vijiko vya supu 2

 

bananas

 

honey

 

NAMNA YA KUTAYARISHA

1.  Kata kata ndizi na stroberi na uweke kwenye mashine (blender) pamoja na vipimo vyote vilivyobaki.

2.  Saga mchanganyiko wako hadi ulainike vizuri.

3.  Mimina kwenye gilasi na itakuwa tayari kwa kunywewa.

 

img

 

ENJOY 🙂

Kinywaji: Juisi ya Embe

VIPIMO

 

Maembe yaliyoiva                                  2

Mtindi (yogurt)                                      2 Vikombe vya chai

Maziwa                                                 1 Kikombe cha chai

Asali au Sukari                                       ¼ Kikombe cha chai

Maji ya ndimu                                        ½ Kipande

Barafu                                                    12 vipande

Mdalasini ya unga                                   kidogo

   juicy-red-mango-yali-shi

 Mango-1-Cropped

NAMNA YA KUTAYARISHA

 

  1. Menya maembe yako kisha ukate kate vipande.
  2. Weka vipimo vyote vilivyopo hapo juu isipokuwa mdalasini, kwenye mashine ya kusagia (blender).
  3. Saga hadi ilainike.
  4. Mimina kwenye gilasi na unyunyize mdalasini kidogo
  5. baada ya hatua hizo juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa

011

ENJOY 🙂