Upishi wa Tambi za Kukaanga

VIPIMO

Tambi                                        pakti moja

Sukari                                       ¾ kikombe cha chai

Mafuta                                       ½ kikombe cha chai

Iliki                                             kiasi 

Maji                                           3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose                    1-2 Tone

Zabibu                                       Kiasi (Ukipenda)

0112 0181 0391 Tambi za kukaanga

NAMNA YA KUTAYARISHA NA  KUPIKA

 

1.    Zichambue tambi ziwe moja moja.

2.    Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina  

      tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

3.    Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

4.    Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki  

      na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari

      koroga kidogo na punguza moto.

 5.    Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili  zikaukie vizuri. 

6.    Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

 

Kidokezi   Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza   kuongeza maji kidogo.