Upishi wa keki ya maziwa

MAHITAJI
 
Unga wa ngano                            240 gram
Baking Powder                             1-½ kijiko kidogo cha chai
Salt                                                ¼ kijiko kidogo cha chai
yai zima                                        5 , kisha tenganisha ute wa njano na mweupe
Sukari                                           240gram  , gawa nusu pembeni
Vanilla                                          1 kijiko kidogo cha chai 
Maziwa ya maji                           30 gram
Evaporated Milk                          kopo 1
Sweetened au Condensed Milk   kopo 1
Cream nzito kabisa ( Heavy Cream)  60gram


KWAJILI YA ICING (kupamba): 

Heavy Cream, kwajili ya kupambia         kijiko 1 kikubwa cha chakula 
Sukari nyeupe ya unga                              kijiko 1 kikubwa cha chakula 

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi :
Saa 1 mpaka masaa 2 

Muda wa mapishi : Dakika 30 mpaka saa 1 
Ukubwa na Idadi : utapata cake 2 
Washa kwanza oven kwa moto wa 350 degrees. Kisha chukua tray yenye size hii 9 x 13 inch unaweza paka siagi au ukaspray. Kisha chukua unga changanaya na baking powder pamoja na chumvi katika bakuli kubwa.

 
Kisha chukua bakuli safi na kavu weka ute wa yai wa njano pamoja na sukari 180 gram piga kwa kutumia mchapo kwa nguvu sana au kama unatumia mashine basi weka spidi kali.

 
Hakikisha inakua muonekano huu baada ya kupiga na mshine unapata rangi ya cream.

 

Kisha chukua yale maziwa ya maji pamoja na vanilla kisha chukua mwiko huo na changanya pole pole mpaka vyote vichanganyike vizuri.
 

 

Kisha chukua ute mweupe wa yai (egg whites) piga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali mpaka uone imetoa mapovu kabisa na kuongezeka. 

 

Baada ya kutoa povu basi chukua sukari 60 gram na mimina katika mchanganyiko huo wa ute mweupe wa yai.

 

Endelea kupiga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali hakikisha imekua laini kabisa kama mapovu lakini isikwe kavu.

 

Unaona muonekano baada ya kua katika kiwango safi na imetengeneza kama milima miwili?

 

Chukua ule mchanganyiko mweupe wa yai changanya pamoja na mchanganyiko ule wa unga.

 

Hakikisha unachanganya pole pole
 
Mpaka ichanganyike vizuri kabisa.
 

 

Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ulioandaa kwajili ya kuokea hakikisha unasambaza vizuri.
 
Choma kwa dakika 35 mpaka 45 au mpaka toothpic ukitoa inabaki kavu. Mara yangu ya kwanza kuipika keki hii nilifungua oven zaidi ya mara 100 ambayo ni kosa sababu ya harufu nzuri ilioenea jikoni kila muda nahisi labda imeshaiva! Nadhani ndio maana keki yangu ilinywea hahahahaaaa! usifanye kosa hili ingawa taste yake ilikua YUMMO!
 

 

Keki yako tayari inarangi safi sana ya kahawia kisha chukua condensed milk, evaporated milk pamoja na heavy cream changanya.
 

 

Hakikisha unachanganya pole pole mpaka ichanganyike vizuri.
 
Baada ya keki yako kuiva weka pembeni ili ipoe na ikishapoa, Chukua uma na uitoboe pole pole . 

 

KIsha chukua mchanganyiko huo wa nmaziwa na cream mwagia juu ya keki na uruhusu ipoe kwa dakika 30. Weka kwenye friji ili ipate ubaridi kabisa isisumbue unapoipamba na icing. Chukua  heavy cream na vijiko 3 vyasukari kisha piga pamoja. 
 
Hakikisha unapiga mpaka inalainika kabisa.

 

Hakikisha unapakaza vizuri icing yako juu ya keki yote ili kuongeza ladha, ingawa mimi huwa nagawa nusu napaka na nusu sipaki maana sio watu wote wanapenda cream. Umeona muonekano baada kukata kipande? Unaona muonekano wa maziwa sehemu tuliokata kipande cha keki? maziwa unayoweka katika hii keki hayatabadiklisha sana keki yako iwe tepe tepe bado itakua na hali ya sponji.

 

Keki hii asili yake ni nchi ya spain wao wanapenda sana kupambia kwa juu matunda aina ya peaches na cherries. Kwakua ilikua ni msimu wa maembe mi nikaona kwanini nisipambie maembe ?!

 

Baada ya kupaka cream kwa juu kisha pamba na maembe na kata vipande kama muonekano katika picha.

 

Ukitafuna utaona sponji safi kabisa na ladha safi
 

 

Pia hata hotelini unaweza kuuza keki hii kama chakula kitamu baada ya mlo kamili
 

 

Waandalie nyumbani waweze kufurahia keki hii kwa chai ya jioni au baada ya chakula.

Upishi huu Umeandaliwa kwa hisani ya : http://activechef.blogspot.com.tr/