Upishi wa chapati: Mkate wa kusukuma

Vipimo:

 • Unga wa ngano mweupe                       1 Kilo
 • Samli (mafuta)                                        150gm
 • Chumvi                                                   3 vya chai
 • Maji ya moto yasichemke lakini               Kiasi
 • Mafuta Ya Zaituni                                     4 vijiko vya supu
 • Samli tena                                                200 gms
 • Iliki (Hiliki) iliyosagwa                               1 kijiko cha chai

 670px-Make-Chapati-Step-5

 20120510-chapati-wraps-with-liver-1 chapati17

Namna ya kutayarisha na kupika:   

(1) Tia unga  kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.

(2) Uunga uwe  mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 60 (saa moja hivi) ukiwa umeufinika ili unga ulainike. 

(3) Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa  ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa nusu saa ukiwa umefinika bila ya kuingia upepo ndani.

(4) Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo   hata chupa  kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.  

(5) Yayusha samli nyingine ya 200gm  kisha itumie kwa kupaka kwenye kila donge ukilisukuma duara itakayobakia weka kando utachomea chapatti.

(6) Likate katikati kwa kidole chako au kijiko upate mgawanyo wa sehemu mbili sasa kila sehemu utakunja kwanzia ncha moja hadi ikutane na ncha nyengine kama mkeka, donge lake linakuwa na sampuli, huitwa tabaki 

(7) Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.

(8) Sukuma kila donge  kisha mara nyengine mviringo huu utakuwa mviringo wa kuchoma weka chapati kwenye chuma kavu bila samli  iache muda wa dakika tatu igeuze upande mwengine kisha vilevile ,  ukiona ina mabapa ya kuchomeka tia samli ile uloyeyusha kwa kijiko kikubwa kimoja huku unaizungusha zungusha.  

(9) Geuza upande wa pili vile vile mpaka iwive.

(10) Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.

6693984chapati

Kidokezo:

Ukipenda kuzichambua kidogo chapati baada ya kumaliza hii unazishika zote kwa pamoja ikiwa umezikunja, unakunja ngumi au kifimbo kupiga tu mara moja tosha.

 

Make a Donation Button

Upishi wa Katles

MAHITAJI

A. Nyama ya kusaga                          Kilo 1

B. Viazi mbatata                                

C. Giligilani

D. Swaum, tangawizi, hoho, keroti

E. Chumvi kiac, ndimu

F. Binzari nyembamba, pilipili manga

G. Mayai                                            4

H. Unga wa sembe/ngano

I. Mafuta ya kupikia uyapendayo

MAANDALIZI

10357453_906927532657029_6364466533463430818_n katlesi za nyama-310409719_906927652657017_3422456731266258448_n

Hatua Ya Kwanza

Chukua nyama yako ya kusaga weka katika sufuria, weka chumvi kiasi, tia ndimu, kitunguu swaum, tangawizi na iache ichemke. Usiweke maji hata kidogo itaiva yenyewe na yale maji maji yake na uhakikiche yale maji yamekauka kabisa. Ipua na uweke pembeni ukisubiri ipoe usisahau kuonja kujua kama viungo vipo sawa.

 

Hatua Ya Pili

Menya viazi vyako mbatata na usafishe vizuri, baada ya hapo vikate kate na uviweke kwenye sufuria yako, Tia chumvi kiasi, tangawizi kiasi, virushe rushe na uweke jikoni tia na maji kiasi, funika na acha vichemke kwa muda (ila mimi napendelea kuweka na maji kiasi ili yakaukie kabisa hua sipendi baada ya viazi kuwiva nichuje maji). Vikisha iva na make sure havina maji anza kuvisaga, utaendelea kusanga mpaka upate ulaini unaoutaka wewe.

 

Hatua Ya Tatu

Katakata hoho, vitunguu maji, keroti katika mfumo ule ule wa vipande vidogo vidogo na ukimaliza hapo chukua mchanganyiko wako wa nyama na viazi uweke katika chombo kimoja, halafu chukua vitunguu maji, hoho, keroti ulivyo katakata tia kwenye mchanganyiko wako wa nyama na viazi, tia swau yako, kamulia tena ndimu, weka na unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, katia na giligilani zako, sasa anza kuchanganya vyote kwa pamoja. Changanya chananya mpaka utakapo ona vyote vimechanganyika vizuri. Please test mchanganyiko wako kuoma kama mambo yapo poa.

 

Hatua Ya Nne

Andaa sahani zako za kuwekea madonde yako ya katres zinyunyuzie unga wa sembe ama ngano itategemea wewe wataka unga gani. Waeza tumia unga wa sembe au ngano. Ukisha maliza hapo chukua mchanganyiko wako na utengeneze style uipendayo kama vidualisho, CD-style finger style yote kheri tu. Baada ya hapo utaviviringisha katika unga wako ulio uchagua wewe na utapanga kwenye sahani, utarudia hivyo katika vidude vyote. Next chukua mayai yako yale manne yavunje na kutia katika chombo safi at the same time unakua ushabandika kichomeo chako jikoni na ushaweka mafuta yako. Tumia moto wa wastani . Mafuta yakishapata moto kiasi cha wewe kuridhika chukua katres zako tia katika mayai zungusha zungusha ili mayai yaingie pande zote then tia kwenye kikaangio chako jikoni, rudia kafanya hivyo kwa katres zote zilizo baki na ukimaliza hapo mambo yatakua poa na tayari kujisevia.

 

Unaweza pia kusoma upishi huu kupitia Alhidaaya: http://www.alhidaaya.com/sw/node/2774

Supu Ya Kuku Na Viazi/Mbatata

VIPIMO :

Kuku                                                            4 LB

Viazi/mbatata                                              3

Kitunguu maji                                               1

Kitunguu thomu                                            5 chembe

Pilipili mbichi                                                  2

Nyanya ya kusaga                                       1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga                                    ½  kijiko cha chai

Haldi/tumeric/bizari ya manjano                    ¼  kijiko cha chai

Mafuta ya zaytuni                                         2 vijiko vya supu

Kotmiri (coriander freshi)                              1 msongo

Ndimu/siki                                                    2 vijiko vya supu

Chumvi                                                        kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 1. Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
 1. Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.
 1. Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
 1. Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.
 1. Kisha  tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.
 1. Tia nyanya,  haldi, na maji kiasi.
 1. Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
 1. Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.
 1. Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa  na mkate au upendavyo